VINARA wa Ligi Kuu England, Manchester City hawaamini macho yao baada ya kubanwa mbavu na Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Selhurst Park ulisoma Crystal Palace 0-0 Manchester City na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.
Sare hiyo inawafanya City kufikisha alama 70 wakiwa nafasi ya kwanza huku Crystal Palace wakiwa na pointi 34 nafasi ya 17 katika msimamo wote wamecheza mechi 29.
Ni Liverpool ambao walikuwa wakiifuatilia mechi hiyo kwa ukaribu wao wapo nafasi ya pili na pointi 66 tofauti ya alama nne kulingana na City ambao ni vinara.
Liverpool wao wana mchezo mmoja mkononi dhidi ya Arsenal unatarajiwa kuchezwa kesho hivyo mbivu na mbichi zitajulikana kesho itakuajekuaje.