SHABIKI wa Yanga kutoka Morogoro aliyeahidi kumzawadia mchezaji Fiston Mayele Ng’ombe mmoja baada ya kufunga bao katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, ametimiza ahadi na kumfikisha Ng’ombe huyo leo Machi 14, 2022.
Ni katika makao makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam zawadi imefika kwa ajili ya kutimiza ahadi ya muda kidogo.
Mayele alipewa ahadi ya kupewa Ng’ombe na shabiki huyo, baada ya kufunga bao katika mechi iliyochezwa Februari 23, mwaka huu katika Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Pia shabiki huyo amekabidhi mbuzi mmoja kwa ajili ya Rais na Mkurugenzi wa GSM, Ghalib Said Mohamed, ikiwa ni pole kwa kufiwa na baba yake mzazi, Said Mohamed.