LICHA ya kupata pointi moja mbele ya Mtibwa Sugar bado Tanzania Prisons inabaki palepale ilipokuwa nafasi ya 16 baada ya kucheza mechi 17.
Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Prisons 0-0 Mtibwa Sugar.
Mtibwa Sugar pia inafikisha pointi 16 katika msimamo ipo nafasi ya 12 na imecheza mechi 17.
Prisons haijawa na mwendo mzuri kwa msimu wa 2021/22 baada ya kucheza mechi 17 imekusanya pointi 13.
Ni mechi 3 pekee imeshinda na sare imekusanya 4 huku ikiambulia kichapo katika mechi 10 na safu yake ya ushambuliaji imetupia mabao 9 kibindoni.
Kinara wa ligi ni Yanga mwenye pointi 42 baada ya kucheza mechi 16 msimu wa 2021/22.