LIVERPOOL ni mabingwa mara 9 wa Carabao Cup na usiku wa kuamkia leo waliweza kufikisha taji lao hilo la 9 muhimu.
Ni ushindi wa penalti 11-10 dhidi ya Chelesea baada ya dakika 120 kukamilika bila kupatikana mbabe kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Wembeley.
Mipango ya Kocha Mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel kumuamini Kepa Arrizabalaga katika kuokoa penalti ulikwama kwa kuwa hakuweza kuokoa mchomo hata mmoja.
Ikumbukwe kwamba Kepa aliwahi kufanya hivyo kwenye Europeans Super Cup na Chelsea ilishinda huku Kepa akiweza kuokoa penalti 2 lakini mbele ya Liverpool, mambo yalikuwa tofauti.
Chelsea kwenye mchezo huo iliweza kufanya umiliki kwa asilimia 46 na Liverpool ilikuwa ni kwa asilimia 54.