MZUNGUKO WA PILI UPO KARIBU,KAZI IENDELEE

    NJIA ambayo inatumika katika kusaka ushindi kwa kila timu ni maandalizi mazuri na wachezaji kupambana bila kuchoka ndani ya uwanja.

    Imekuwa hivyo kwa timu ambazo tayari zimekamilisha hesabu za mzunguko wa kwanza na nyingine bado mechi moja mkononi kufanya hivyo.

    Hakuna namna nyingine inayotakiwa kufanyika zaidi ya kila timu kuweza kufanya maandalizi mazuri kwa kuwa kila anayeingia kwenye ushindani anahitaji kupata pointi tatu.

    Kikubwa ambacho nina amini kwamba kwa sasa kwenye ligi hakuna mnyonge. Kila mmoja ni shujaa na anaweza kupata matokeo ambayo anayahitaji awe nyumbani ama ugenini.

    Namna ambavyo timu itaamua kufanya basi itapata matokeo ya kile ambacho inakihitaji kama ni ushindi sawa kama ni sare huwa pia kwa kuwa kila kitu ni mipango.

    Tumeshuhudia timu zikipata matokeo chanya licha ya kwamba zilikuwa hazipewi nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zao. Pia zipo ambazo zilifanya vibaya licha ya wengi kufikiria kwamba zitapata matokeo.

    Hali halisi ilikuwa ni kushindana katika kila namna. Mzunguko wa kwanza umekuja na picha ya kipekee na kuonyesha kwamba ikiwa kila timu itakuwa makini ni rahisi kufikia malengo.

    Zile ambazo zimekamilisha mzunguko wa kwanza ni muda wa kufanya maandalizi kwa ajili ya mzunguko wa pili na zile ambazo bado zina kazi ya kukamilisha hesabu za mzunguko wa pili kwa umakini.

    Kuanzia wamiliki wa timu, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenyewe wameona namna hali halisi ilivyo ndani ya ligi kwa mzunguko wa kwanza.

    Hakuna timu ambayo haileti ushindani uwanjani hili ni jambo kubwa na la kuzingatia. Ikiwa kila timu inaleta utofauti ndani ya ligi inaongeza uimara na ubora wa ligi yet ambayo ni pendwa.

    Sasa ambacho kinatakiwa ndani ya uwanja kwa wachezaji ni kupambana kwa hali na mali kupata matokeo. Kwa benchi la ufundi ni wakati sahihi wa kufanya tathimini ya kile ambacho wamekipanda.

    Ukweli ni kwamba kila timu inajua pale ambapo iliboronga kwenye mzunguko wa kwanza. Muda huu wa kuelekea kwenye mzunguko wa pili ni lala salama na kila timu inatakiwa kujipanga sawasawa.

    Kama ilikuwa inashindwa kupata matokeo chanya ndani ya dakika 90 itazame kwa uzuri namna gani inaweza kujiboresha zaidi.

    Yale makosa ambayo yalikuwa yanajirudia kwa timu na kupoteza mechi zao ni wakati wa kuziboresha. Wale ambao walikuwa wanakosa matokeo ndani ya uwanja wanatakiwa kubadili mbinu na kuboresha zaidi yale makosa kutokuwepo.

    Hakuna muda wa kupoteza tena kwa sasa ndani ya uwanja kwani muda hausubiri unakwenda mbele. Muhimu kujua malengo ambayo yamewekwa kwa timu kiujumla pamoja na wachezaji.

    Ipo wazi kwamba yule ambaye hatashtuka kwa wakati huu kila mmoja atakuwa na safari yake ya kusaka ushindi ndani ya uwanja.

    Kwa kuyafanyia kazi makosa yaliyopita itatoa mwanga kwa timu kuanza upya na kufanya vizuri kwenye mechi zilizobaki. Uhakika wa kupata matokeo baada ya dakika 90 ni muhimu kwa kila timu.

    Kitu pekee ambacho kinaweza kuzifanya timu zibaki ndani ya ligi kwa msimu ujao ni kupambana na kusaka matokeo ndani ya uwanja.

    Chaguo la kufanya vizuri lipo mikononi mwa timu zenyewe kwa wakati huu. Inawezekana na ipo wazi kwamba kila timu ina nafasi ya kushinda mechi zilizobaki.

    Previous articleMarioo – YANGA Tamu (Official Video)
    Next articleVIDEO:MANENO YA KOCHA WA ZAMANI WA AZAM FC,ATAJA UGUMU ULIVYO