YANGA YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA MBEYA CITY
UWANJA wa Mkapa dakika 90 zimekamilika kwa timu zote kugawana pointi mojamoja kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. Ubao umesoma Yanga 0-0 Mbeya City na kufanya Mbeya City wachezaji wa timu hiyo kushangilia. Yanga inafikisha pointi 36 kibindoni huku wakiwa hawajapoteza mchezo kwa msimu wa 2021/22.