AZAM FC itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Azam Complex.
Azam FC ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 21 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 8 na pointi 17.
Kesho Februari 4 kutakuwa na mchezo kati KMC v Biashara United.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex
Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 15 inakutana na Biashara United iliyo nafasi ya 15 na pointi 11.
Kinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni Yanga mwenye pointi 35 baada ya kucheza mechi 13.