Home Sports MORRISON,ONYANGO MIKATABA YAO YAWEKWA KANDO SIMBA

MORRISON,ONYANGO MIKATABA YAO YAWEKWA KANDO SIMBA

MAMBO ni magumu kwa sasa ndani ya Simba kutokana na mwendo wa kusuasua hasa kwenye matokeo waliyopata kwenye mechi tatu mfululizo ugenini jambo lililofanya mikataba ya mastaa wengi kuwekwa kando.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya Simba zimeeleza kuwa kwa sasa hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ameitwa kufanya mazungumzo kuhusu kuongeza mikataba yao ili waweze kuhudumu ndani ya kikosi
hicho.


Miongoni mwa mastaa ambao 
mikataba yao inatarajiwa kufika ukingoni pale msimu wa 2021/22 utakapomeguka ni pamoja na Bernard Morrison, Hassan Dilunga, Ibrahim Ame, Joash Onyango na Said Ndemla.


Hii ni sawa na Simba kuwaweka 
sokoni nyota wao ambao wamebakiza mkataba wa chini miezi sita kwani kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘Fifa’ mchezaji anapobakiza muda huo kwenye kandarasi yake anakuwa huru kufanya mazungumzo na timu nyingine yoyote na wakikubaliana anaweza kusaini mkataba wa awali.


Baada ya taarifa kueleza kwamba 
hakuna mpango wowote ambao unaendelea kwa sasa, Championi Jumatano lilimtafuta Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ili aweze kuzungumzia suala hilo simu yake haikupokelewa.


Alipotafutwa Mwenyekiti wa Simba, 
Murtanza Mangungu azungumzie ishu hiyo pia hakupatikana.

Previous articleRATIBA YA LEO LIGI KUU BARA
Next articleTANZANITE KATIKA KIBARUA KIZITO LEO