SIMBA YASHINDA KWA PENALTI MBELE YA PRISONS
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo wepata ushindi mbele ya Tanzania Prisons baada ya mechi tatu za ugenini kushindwa kupata matokeo. Bao la ushindi limepachikwa na Meddie Kagere baada ya mwamuzi wa kati kuamua ipigwe penalti ambayo ilikuwa ikionekana kupingwa na wachezaji wa Prisons. Jumla Simba inakuwa imefunga mabao 15 katika mechi 14…