>

SPORTPESA YAZINDUA MULTIBET BONUS YA KIBABE

KAMPUNI ya michezo na burudani Sportpesa inayo furaha kutambulisha kwa Watanzania, huduma yake
mpya ya Multibet Bonus kwa wachezaji wake wote nchini.

Bidhaa hii ni ya kwanza na ya kipekee kwa wachezaji wao kutokana na kiwango cha asilimia ambacho mteja atakuwa anakipata baada ya kuweka ubashiri wake kwa mechi kuanzia 3.

Sportpesa imefungua mwaka kwa kishindo, kwa kuwaongezea wateja wao kiwango cha asilimia za mapato kwenye odds, kwenye mechi watakazokuwa wanachagua na kuweka kwenye bashiri zao wakati wa kupanga mikeka yao.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Sportpesa, Tarimba Abbas amesema:-“Wachezaji wetu watapata bonasi mpaka asilimia themanini na tano (85%)ya kiasi ya kubet kulingana na idadi ya timu watakazochagua katika bashiri zao.

“Wachezaji watakaoruhusiwa kushiriki fursa hii ni wale watakaokuwa wanabashiri na Odds zisizopungua 1.2 na timu za kuchagua zisizopungua tatu.

“Tunajua kuna wachezaji wetu wanaopenda kucheza mechi nyingi,
hivyo basi huduma hii imelenga kuwaongezea chachu ya kucheza mechi nyingi zadi kadiri wawezavyo ili wapate zaidi kama asilimia
zitakavyojiongeza.

Aidha, bidhaa hii ya Multibet Bonus, itakuwa inapatikana kupitia
Sportpesa App yetu, inayopatikana kwa watumiaji wa simu janja na pia kupitia website yetu ya www.sportpesa.co.tz, kwa wanaotumia kompyuta mpakato pekee.

“Huduma hii ya Multibet Bonus, ni moja ya bidhaa bunifu, kutoka kwetu ambayo itakuwa inapatikana kwenye mechi za kila siku.

‘’Haya ni maboresho ambayo kampuni imeamua kuyaongeza katika
kukupa wewe mteja ama mchezaji fursa ya kupata zaidi katika kila
ubashiri utakaokuwa unaouweka.

“Sambamba na bidhaa hii, Sportpesa inajitahidi kuboresha huduma zake zote ili ziweze kukidhi malengo na matakwa ya wachezaji wake, pamoja na soko kwa ujumla, kwa kiwango cha juu kabisa,” amesema Tarimba.