KUTOKANA na kitendo chake cha kupoteza muda mwamuzi wa kati Nassoro Mwinchui aliweza kumuonyesha kadi ya njano kipa Shaban Kado.
Mbali na kadi hiyo aliweza kutimiza majukumu yake vema akiwa na jezi ya Mtibwa Sugar wakati wakiibana Simba kushindwa kupenya katika ngome za Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu na alitumia dakika zote 90.
Kado alikuwa ni mchezaji bora wa mchezo wakati wakigawana pointi mojamoja kutokana na umakini wake wa kuokoa hatari.
Ilikuwa ni dakika ya 18,31,36,39,47 na 76 aliwez kufanya yake na hatari kubwa ilikuwa ni ile ambayo aliifanya Abdi Banda wakati wa kuokoa ila Kado aliweza kusepa nayo.
Kado amesema kuwa bado yupo na ataendelea kuwepo katika ubora kwa kuwa anaipenda kazi yake.
Licha ya uwepo wa Meddie Kagere, Cris Mugalu, Pape Sakho na Clatous Chama bado Kado alikuwa ni shujaa katika mchezo huo.