PABLO AZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MTIBWA

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema kuwa kwa namna yoyote ile wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Manungu.

Mtibwa Sugar wameamua mchezo huo uchezwe katika Uwanja wa Manungu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 25,000 na tayari tiketi zimeanza kuuzwa na kiingilio ni 10,000.

Kwenye taarifa ambayo wametoa kuhusu viingilio wameweka wazi kwamba mashabiki wanapaswa kuwahi kuweza kununua tiketi kwa kuwa ni chache na watu wanahohitajika pia ni wachache.

Pablo amesema:”Tunahitaji pointi tatu na tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari hasa ukizingatia kwamba tunajua mchezo wetu uliopita hatukupata pointi.

“Ni timu nzuri ambayo tunakutana nayo tumejipanga kufanya vizuri kupata matokeo chanya, wachezaji wapo tayari na maandalizi yapo vizuri,” .

Mchezo uliopita Januari 17,2022 Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City inakutana na Mtibwa Sugar iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting.