SIMBA KITUO KINACHOFUATA MANUNGU

BAADA ya kurejea Dar wakitoka Mbeya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kituo chao kinachofuata ni Manungu.

Chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco, Januari 17,2022 alishuhudia ubao wa Uwanja wa Sokoine ukisoma Mbeya City 1-0 Simba na mtupiaji alikuwa ni Paul Nonga dakika ya 19.

Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hiyo kupoteza ndani ya Ligi Kuu Bara na ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zake ni 24 huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi 32 na wamecheza mechi 12.

Kazi inayofuata ni kusaka pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar,Januari 22 katika Uwanja wa Manungu mjini Morogoro.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kwamba bado hesabu zao ni kuweza kupata ushindi katika mechi zijazo.

Kwa upande wa Thobias Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amebainisha kwamba watapambana kupata ushindi.