Home Sports SIMBA YANYOOSHWA NA WAGONGA NYUNDO

SIMBA YANYOOSHWA NA WAGONGA NYUNDO

UWANJA wa Sokoine, Mbeya City wameinyoosha Simba kwa bao 1-0 lililopachikwa na Paul Nonga mapema kipindi cha kwanza.

Haikuwa rahisi kwa Simba kuweza kumtungua kipa namba moja wa Mbeya City, Deogratius Munish ambaye alikuwa kwenye ubora wake mwanzo mwisho.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Aishi Manula jitihada zake za kuokoa michomo hazikuzaa matunda kwa kuwa aliokota mpira mmoja nyavuni na kuifanya timu ya Simba kuyeyusha pointi tatu mazima.

Chris Mugalu kwenye mchezo wa leo alikosa penalti dakika ya 48 baada ya mpira aliopiga kugonga mwamba na mmaliziaji John Bocco pigo lake lilidondoka kwenye mikono ya Dida.

 

Previous articleUWANJA WA SOKOINE, MBEYA CITY 1-0 SIMBA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE