Home Sports YANGA ANAYOITENGENEZA KOCHA NABI NI BALAA!

YANGA ANAYOITENGENEZA KOCHA NABI NI BALAA!

 

KOCHA Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi katika ripoti yake ameagiza kila nafasi ya mchezaji wa kigeni lazima awepo mbadala wake mzawa mwenye uwezo mkubwa kama wake.


Yanga tayari imefanikisha usajili
wa wachezaji watatu wazawa katika usajili wao wa dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka huu ambao unaendelea.

Wachezaji hao wapya waliosajiliwa ni Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ atakuwa mbadala wa Khalid Aucho, Abdoultwalib Mshery yeye mbadala wa Djigui Diarra huku Denis Nkane akichukua nafasi ya Jesus Moloko.


Bosi mmoja mwenye ushawishi
wa usajili katika timu hiyo, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, Nabi na msaidizi wake, Mrundi Cedric Kaze ndiyo wamependekeza aina hiyo ya usajili.


Alisema kuwa kama lengo la
kufanya usajili huo ni kuwepo mbadala wa mchezaji wa kigeni katika kila nafasi ambaye ana uwezo mkubwa ili akikosekana kwa kadi au majeraha, basi benchi la ufundi linakuwa halina hofu.

 

Aliongeza kuwa katika nafasi ya kiungo mkabaji inayochezwa na Yannick Bangala tayari imempata mbadala wake ambaye Zawadi Mauya ambaye amecheza michezo miwili ya ligi katika kiwango bora.


“Kama unakumbuka vizuri
mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alikosekana Bangala baada ya kugua ghafla wakati timu ikiwa katika maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.


“Lakini benchi la ufundi alikuwa
na presha kubwa na badala yake kumtumia Mauya na kucheza vizuri
na kutoonekana pengo lolote katika
timu.


“Hivyo ndiyo ambavyo benchi la
ufundi linataka kutengeneza timu yenye ushindani bila ya kumtegemea
mchezaji mmoja na usajili wa Nkane,
Sure Boy na Mshery wa mipango katika timu,” alisema bosi huyo.


Yanga kwa kupitia mwanasheria
wao, Simon Patrick alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Kocha Nabi
na Kaze wamekuja na ‘philosophy’
itakayolisaidia taifa na timu ya taifa miaka ya hivi karibuni.


“Wamekuwa wakifatilia kwa makini
mechi zote za ligi kuu na daraja la kwanza ili kuviona vipaji, na pale
watakapojiridhisha huwashawishi
viongozi kuchukua vipaji hivyo.

 

“mkakatati wake ni kwamba kila namba yenye mchezaji wa kigeni lazima iwe na mchezaji mzawa kama
‘succession plan’.


“Kinachofuata uwapa mafunzo
maalum na kuwaandaa kupambania namba huku akiwapa fursa kidogo
kidogo, atakayeweza kumshawishi
basi anajipatia namba ya kudumu.”

Previous articleJIONEE PICHA AJIB AKIWA MAZOEZINI AZAM, KUKIWASHA LEO
Next articleAUBA AINGIA ANGA ZA NEWCASTLE UNITED