>

DEUS KASEKE ATAJWA KUSEPA YANGA

IMEELEZWA kuwa kiungo wa mpira mali ya Yanga, Deus Kaseke yupo mbioni kusepa ndani ya kikosi hicho ili akapate changamoto mpya katika timu nyingine.

Mtibwa Sugar inapewa nafasi kuweza kupata saini ya kiungo huyo ambaye kwa sasa hana nafasi kikosi cha kwanza cha Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Leo Januari 4 Yanga inatarajiwa kuibukia Zanzibar kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Ikumbukwe kwamba mabingwa wa taji hilo ni Yanga hivyo wanakwenda kutetea taji lao walilotwaa mwaka 2021 kwenye fainali baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti mbele ya Simba.

Kuhusu wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo hivi karibuni Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli aliweka wazi kwamba wale ambao watatolewa kwa mkopo watatangazwa.