MWAMBA WA LUSAKA KUREJEA SIMBA

IMEELEZWA kuwa kiungo wa mpira Clatous Chama nyota wa RS Berkane yupo njiani kurudi Simba kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Ni msimu uliopita wa 2020/21 Chama alikuwa ndani ya Simba na alikuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Didier Gomes ambaye alibwaga manyanga msimu huu wa 2021/22 baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa zimeeleza kuwa Simba imeamua kumrejesha kwa mara nyingine Chama ili kurejesha muunganiko imara kwenye kikosi hicho hasa eneo la kiungo ambalo limekuwa likipata shida kwenye utengenezaji wa nafasi.

Msimu uliopita aliweza kufunga mabao nane na kutoa pasi 13 za mabao ndani ya Ligi Kuu Bara.