RASMI leo Januari 3,2022 uongozi wa Simba umemtangaza Ahmed Ally kuwa Ofisa Habari wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Pablo Franco.
Ally anakuja kuchukua mikoba ya Haji Manara ambaye alibwaga manyanga mwaka 2021 na sasa ni Ofisa Habari ndani ya kikosi cha Yanga.
Aliposepa Manara nafasi hiyo alikaimu Ezekiel Kamwaga ambaye kwa sasa yupo nje akisoma.
Ally ni mwandishi pia wa Azam TV ambapo amekuwa akiripoti habari za michezo.
Hongera Ahmed Ally katika majukumu yako mapya na kila la kheri.