YANGA imeshinda mabao 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Huu ni mchezo wa kufunga mwaka 2021 ambapo Yanga imefunga kwa aina yake kwa kupata ushindi mkubwa wa mabao zaidi matatu.
Yanga walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Fiston Mayele dakika ya 41.
Kipindi cha pili Yanga iliweza kupachika bao la pili dakika ya 57 ni Jesus Moloko alipachika bao la pili huku bao la tatu ikiwa ni la kujifunga kwa Dodoma Jiji lilifungwa na Justin huku lile la nne likifungwa na Khalid Auho dakika ya 81.
Cleophance Mkandala alifanya jaribio ambalo halikulenga lango kwenye mchezo huo ilikuwa ni dakika ya 89 na lilikwenda nje ya lango.
Yanga inaongoza ligi na inafunga mwaka 2021 ikiwa ni namba moja na pointi zake ni 29.