NYOTA Omary Muvungi kutoka kituo cha mpira wa miguu cha Cambiasso Sports, Omary Mvungi amefanikiwa kwenda nhini Uingereza kwa mwaliko kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Chelsea Denis Wise.
Nyota huyo ambaye ni mshambuliaji alipata fursa pia ya kupiga picha na mchezaji huyo na nahodha wa zamani wa Chelsea, Dennis Wise baada ya kutua nchini Uingereza.
Taarifa iliyotolewa na Cambiasso kupitia Ukurasa wake rasmi wa Instagrama imeeleza; “Cambiasso Sports Management tukishirikiana na Rainbow Sports tumefanikiwa kumpeleka striker wetu kinda wa Cambiasso Sports Academy na timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20 nchini Uingereza kwa mwaliko wa aliyekuwa mchezaji nguli na Nahodha wa Chelsea na Timu ya Taifa ya Uingereza Denis Wise kwa ajili ya kupata mafunzo na misingi bora kwa ajili ya maandalizi ya kucheza soka la kulipwa (PROFESSIONAL FOOTBALL) barani Ulaya,”.
Hii ni hatua kubwa kwa soka la Tanzania kwa kufungua njia kwa vijana na kuonyesha kwamba mpira ni ajira na vipaji vipo kwenye ardhi yetu hii pendwa.