Home Sports BREAKING:IBRAHIM AJIBU APEWA MKONO WA KWA KHERI SIMBA

BREAKING:IBRAHIM AJIBU APEWA MKONO WA KWA KHERI SIMBA

BREAKING:UONGOZI wa Klabu ya Simba umethibitisha kusitisha mkataba wa kiungo fundi Ibrahim Ajibu.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Simba imeeleza kuwa imefikia makubaliano ya pande zote mbili kwa maslahi mapana kusitisha mkataba wa kiungo huyo mshambuliaji.

Ajibu alirejea nyumbani kwa mara nyingine tena akitokea Yanga ambapo alipokuwa huko alikuwa ni nahodha na alipofika Simba mambo yalikuwa magumu kwake.

Jana Desemba 29 wakati wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi Uwanja wa Bunju Complex kujiaandaa na mchezo ujao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Januari Mosi 2022 Uwanja wa Mkapa hakuwepo mazoezini.

Previous articleMTANZANIA ATUA ULAYA KUBORESHA MISINGI
Next articleAZAM FC YAPATA MRITHI WA SURE BOY ALIYESAINI YANGA