>

KIPA SIMBA ATAJWA KUIBUKIA MTIBWA SUGAR

JEREMIA Kisubi kipa namba nne wa Simba ambaye aliibuka hapo akitokea kikosi cha Tanzana Prisons anatajwa kuibuka ndani ya Mtibwa Sugar.

Habari zinaeleza kwamba nyota huyo ameomba atolewe kwa mkopo ili aweze kupata changamoto mpya kwa kuwa ndani ya Simba hana nafasi ya kuanza kwenye mechi za ushindani.

Mpaka sasa Simba ikiwa imecheza mechi 9 ndani ya Ligi Kuu Bara hajapata nafasi ya kuanza kiksosi cha kwanza kwenye mchezo hata mmoja na ni kipa nama moja Aishi Manula ameweza kukaa langoni kwenye mechi zote hizo.

Mtu wa karibu wa kipa huyo amesema kuwa Kisubi anahitaji kwenda kucheza Mtibwa Sugar kwa kuwa tayari kipa wa Mtibwa Sugar, Aboutwalib Mshery amesaini dili jipya ndani ya Yanga.

Jana kwenye mazoezi ambayo yalifanyika Uwanja wa Bunju Complex hakuwepo sehemu ya kikosi kilichokuwa kikifanya maandalizi ya kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Januari Mosi 2022.