>

VIGOGO SIMBA WAKOMALIA ISHU YA CHAMA

VIGOGO wa Kamati ya Usajili ya Simba, chini ya Mtendaji Mkuu (C.E.O.) wa timu hiyo, Barbara Gonzalez, wameona isiwe shida na kuchukua maamuzi ya kupanda ndege kumfuata kiungo wao mchezeshaji Mzambia Clatous Chama anayekipiga RS Berkane ya nchini Morocco.


Kiungo huyo anawindwa vikali na Yanga katika
usajili huu wa dirisha dogo lililofunguliwa Desemba
16, mwaka huu kwa ajili ya kukiboresha kikosi 
hicho.


Simba imepanga kukiboresha kikosi hicho katika 
dirisha dogo ambalo inaelezwa tayari imemalizana na winga wa Zanaco, Mzambia Moses Phiri.Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa haraka mabosi wa Simba wamechukua maamuzi ya kumfuata Chama Morocco kwa ajili a kufanikisha dili lake.

Bosi huyo alisema kuwa tayari uongozi huo ulishafanya mazungumzo na wazazi wa Chama walipokwenda kucheza mchezo wa Kombe la ShirikishoAfrika dhidi ya RedArrows ya nchini Zambia.


“Mazungumzo yetu na Chama yanakwenda 
vizuri, mtendaji wetu Barbara na baadhi ya viongozi wa kamati ya usajili wapo safarini kuelekea Morocco kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

“Dili hilo muda na wakati wowote litafanikiwa, kwani viongozi hao wapo Morocco kwa ajili ya kuzungumza na Berkane iliyomsajili katika msimu huu.

“Safari hiyo ya Barbara haitaishia kwa Chama pekee kwani pamoja na kuwepo kwa dili hilo, tayari kuna nyota mwingine ambaye ni kiungo mkubwa tu anaweza kutua kwa ajili ya kuziba pengo la Lwanga kipindi hiki ambacho yeye ana majeraha ya goti ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu,” alisema bosi huyo.


Simba kwa kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi 
ya Wadhamini wa timu hiyo, SalimAbdallah ‘Try Again’ilisema: “Sisi Simba ndiyo wenye nafasi kubwa ya kumsajili Chama, kwani katika mkataba wake kuna masharti tuliyokubaliana nayo ambayo kama ataachana na Berkane, basi Simba ndiyo tutapewa kipaumbele.”