>

YANGA YAFUNGUA MABOX KWA KUIMALIZA BIASHARA UNITED KWA MKAPA

2021 kikosi cha Yanga kimefungua maboksi ya zawadi ya Christmas kwa ushindi mbele ya Biashara United ya Mara.

Dakika 90 zimekamilika Uwanja wa Mkapa kwa ubao kusoma Yanga 2-1 Biashara United.

Biashara United walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 2 kupitia kwa Atupele Green wakashindwa kulilinda.

Bao la usawa kwa Yanga lilipachikwa kimiani na dakika ya 39 na Fiston Mayele na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa wametoshana nguvu.

Bao la ushindi limefungwa na Said Ntibanzokiza dakika ya 79 kwa mkwaju wa penalti.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuwa namba ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza mechi 10.