>

RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO DESEMBA 24

BAADA ya mchezo wao uliopita dhidi ya Kagera Sugar kuahirishwa kutokana na asilimia kubwa ya wachezaji wa Simba kuumwa mafua na homa leo wanatarajiwa kuwa kazini.

Desemba 24, Simba inatarajiwa kukaribishwa na Wanakino Boys, Uwanja wa Al Hassan Mwinyi, Tabora.

Itakuwa ni KMC v Simba leo.

Pia Coastal Union iliyotoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Biashara United itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Mbeya City iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC.

Mchezo wao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.