Home Sports CHAMA MIKONONI MWA BARBARA SIMBA

CHAMA MIKONONI MWA BARBARA SIMBA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa, ishu nzima ya usajili wa majembe mapya kwenye kikosi cha timu hiyo
akiwemo kiungo Mzambia,
Clatous Chama kwa sasa inashughulikiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez.
Chama aliuzwa na Simba
miezi minne iliyopita na kujiunga na RS Berkane ya Morocco akisaini mkataba wa
miaka mitatu unaotarajiwa
kukamilika 2024.


Akizungumza na Spoti
Xtra, kuhusu ujio huo wa Chama na mipango ya usajili ya Simba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema: “Kama ambavyo tuliweka wazi kwa Wanasimba katika mkutano wetu mkuu kuwa tumejipanga kufanya usajili mkubwa ambao utatusaidia kutimiza malengo yetu hasa katika mashindano ya kimataifa.

“Kuhusiana na suala la usajili wa Chama, hili ni suala ambalo CEO wetu Barbara Gonzalez analishughulikia na yeye
ndiye atakayetoa taarifa zote
kuhusiana na masuala ya usajili kwenye kikosi chetu.”


Kwa upande wa Kocha Mkuu
wa RS Berkane anayoichezea Chama, Florent Ibenge, amesema: “Chama ni mchezaji halali wa RS Berkane, bado ana mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hii, kuhusu kuomba kuvunja mkataba,
benchi la ufundi na hata
viongozi wa Berkane hakuna ambaye anazo taarifa juu ya jambo kama hilo, naamini
Chama atasalia hapa.


“Kwa upande wangu kama
kocha bado nina mipango na Chama ya kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri msimu huu katika mashindano mbalimbali ambayo tunashiriki.”

Previous articleVIDEO: SIMBA QUEENS YAIFUNGA 15-0 RUVUMA QUEENS – LIGI KUU YA WANAWAKE, UWANJA wa MO ARENA..
Next articleBOSI YANGA AFUNGUKA WALIVYOMNASA SURE BOY