IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi wapo kwenye hesabu za kumsaka winga wa kazi ili awe ndani ya kikosi hicho.
Yanga inahitaji kufanya maboresho kidogo kwenye eneo la winga ili kuongeza makali kwenye kikosi hicho.
Jina na Chico Ushindi winga mwenye miaka 25 anayekipiga ndani ya TP Mazembe anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Yanga ili aweze kuibuka ndani ya kikosi hicho.
Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha hivi karibuni alisema kuwa kwenye upande wa usajili watasubiri ripoti ya Nabi inahitaji nini.
“Ripoti ya kocha itaamua nini kifanyike hivyo mambo yakiwa sawa taarifa zitatolewa,”.