FT: YANGA 4-0 IHEFU FC

USHINDI wa mabao 4-0 dhidi ya Ihefu FC Uwanja wa Mkapa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya tatu unawafanya waweze kutinga raundi ya nne.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilipachika mabao 3-0 kipindi cha kwanza na kuwafanya waende vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa vifua mbele.

Watupiaji wa Yanga ni Heritier Makambo ambaye ametupia mabao mawili dk ya 5 na 22 huku lile la tatu likipachikwa na Khalid Aucho dk ya 45.

Makambo alipachika bao la nne na kuweza kufunga hat trick yake ya kwanza msimu wa 2021/22.

Zuber Katwila Kocha Mkuu wa Ihefu FC hakuwa na chaguo kwa kwa alishuhudia vijana wake wakipoteza mchezo wa leo Uwanja wa Mkapa.