UONGOZI wa Pamba SC yenye maskani yake Mwanza umeweka wazi kwamba utaongeza majembe mapya ya kazi kwenye usajili wa dirisha dogo.
Usajili wa dirisha dogo unatarajiwa kufunguliwa Desemba 15 kwa ajili ya timu kuweza kufanya usajili ili kuweza kuongeza nguvu kwenye timu zao.
Kwa mujibu wa Katibu wa Pamba SC, Jonson James amesema kuwa watasajili wachezaji hao ili waweze kufanya kweli kwenye Championship.
“Tunasajili wachezaji ili kuimarisha kikosi chetu kwa sababu kuna mapungufu ambayo yapo kwenye kikosi kwa wakati huu hivyo ni lazima tufanye maboresho.
“Kwa ajili ya mzunguko wa pili tutasajili wachezaji makini ingawa kwa sasa timu ipo vizuri na tunaendelea kujipanga,” amesema.
Chanzo:Championi