Home Sports MESSI AMPOTEZA TENA CRISTIANO RONALDO TUZO ZA BALLON D’OR

MESSI AMPOTEZA TENA CRISTIANO RONALDO TUZO ZA BALLON D’OR

WAKATI Lionel Messi staa anayekipiga ndani ya PSG akitwaa tuzo yake ya Ballon d’Or ya 7 kwa upande wa Wanawake ni Alexia Putellas ametwaa tuzo hiyo.

Alexia ni nahodha wa Klabu ya Barcelona upande wa Wanawake ambapo amesema kuwa katika hilo anajiskia furaha kubwa sana.

Messi amempiku kwa mara nyingine tena mshikaji wake wa karibu, Cristiano Ronaldo anayekipiga ndani ya Manchester United.

Kwa mujibu wa kura inaonyesha kuwa Messi amepigiwa kura 613 anafuatiwa na Lewandowski ambaye yupo nafasi ya pili akiwa amepigiwa kura 580.

Pia nafasi ya tatu ni mali ya Jorginho wa Chelsea ambaye yeye amepigiwa kura 460 na Karim Benzema yupo nafasi ya nne na kura zake ni 239, N’Golo Kate ni namba tano akiwa na kura 186.

Nafasi ya sita hapa amekaa mwamba Ronaldo akiwa ametulia kabisa na kura zake ni 178 huku nyota wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah akiambulia nafasi ya 7 na kura 121.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
Next articleYANGA YAINGIA ANGA ZA MSHAMBULIAJI HUYU MATATA