>

MBEYA KWANZA YAPOTEZA KWA KUCHAPWA NA YANGA

WATOTO wa Mbeya Kwanza leo Novemba 30 hawakuwa na chaguo mbele ya Yanga baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

NBC Premeir Leageu inazidi kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kuwa kila timu inapambana kusaka pointi tatu muhimu jambo ambalo limefanya mchezo wa leo kuwa na ushindani mkubwa.

Mabao ya Yanga yalipachikwa na Fiston Mayele dakika ya 25 na Saido Ntibanzokiza dakika ya 17.

Ushindi huo unaifanya Yanga kujikita kileleni wakiwa na pointi zao 19 na kubaki palepale nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

Mbeya Kwanza watajilaumu wenyewe kwa kuwa kipindi cha kwanza walikwama kutulia na kushindwa kuzitumia nafasi ambazo walizipata.

Lakini kipindi cha pili waliweza kutulia na kucheza kwa kushambulia ila ngome ya Yanga ilikuwa imara pia Mbeya Kwanza wenyewe walikosa umakini.

Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Mbeya Kwanza kupoteza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine na mchezo wa pili kwao kupoteza katika ligi.