DAKIKA 45 YANGA WANAULIZA NYIE HAMUOGOPI

WAKIWA Uwanja wa Sokoine Mbeya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga wanauliza eti :’Nyie Hamuogopi’ baada ya kwenda mapumziko wakiwa vifua mbele.

Dakika 45 zimekamilika na ubao wa Uwanja wa Sokoine unasoma Mbeya Kwanza 0-2 Yanga.

Kipindi cha kwanza Yanga wametawala mchezo ambapo wamefunga mabao mapema kabisa ndani ya dakika 20 za awali.

Ilikuwa ni bao la Said Ntibanzokiza kwa pigo huru akiwa nje ya 18 dakika ya 17 na bao la pili limefungwa na Fiston Mayele.

Mayele amepachika bao hilo dakika ya 25 na kuwafanya Wananchi wawe mbele wakiwa ugenini.