VIWANJA VYETU BADO TATIZO, MABORESHO MUHIMU

  WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara na Championship zikizidi kupasua anga kuna tatizo jingine ambalo linazidi kuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele.

  Ipo wazi kwamba kwa msimu wa 2021/22 kila kona kumekuwa na hamasa kwa ajili ya kuona kwamba kila timu inapata matokeo lakini sehemu za kuchezea asilimia 70 bado hazijawa bora.

  Mpaka sasa kwa Dar unaweza kutaja  viwanja vichache ambavyo ni bora kwa kucheza na vinakupa kile ambacho unakihitaji hapo kila mchezaji huwa anakuwa na nguvu ya kuonyesha kile ambacho anacho.

  Ni Uwanja wa Mkapa pamoja na Uwanja wa Azam Complex hapa ni sehemu pendwa kwa timu zote mbili awe mwenyeji ama mgeni.

  Hata Uwanja wa Uhuru ni bora kwa sehemu ya kuchezea kwa kuwa maboresho ambayo yamefanyika ni makubwa lakini pale ambapo timu zinatoka nje kwenda sehemu nyingine inakuwa ni shida kubwa.

  Uwanja wa Mabatini ambao unatumiwa na Ruvu Shooting, wazee wa mpapaso ni miongoni mwa viwanja ambavyo bado havijawa kwenye ubora wenyewe ambao unahitajika hasa kutokana na kuwa na changamoto kwenye upande wa kuchezea.

  Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwa ligi uwanja huu ulifungiwa ili ufanyiwe maboresho kwa kuwa ulikuwa haujakidhi vile vigezo na uzuri ni kwamba waliweza kufanyia maboresho kisha uwanja ukaruhusiwa kutumika.

  Mtibwa Sugar ni wanapata tabu kwa kuwa walianza kucheza nje ya Uwanja wa Jamhuri,Morogoro na sababu kubwa ni ileile kwamba uwanja huo haujawa bora.

  Hapa katika hili ni lazima litazamwe kwa umakini na kila mmoja aweze kuona namna gani inawezekana kuwa na ubora kwenye uboreshaji wa viwanja vyetu.

  Inawezekana na kila kitu ni mipango mizuri basi ni wakati kwa kila mmoja ambaye anahusika kuongeza nguvu kwenye uwekezaji wa mpira.

  Namna ambavyo wadhamini wanajitokeza kwa wingi na kuweka mkwanja wao mezani ni jambo ambalo inabidi liwashtue hawa wanaotunza viwanja.

  Sehemu ambayo inahitaji kuwa bora na imara ni pamoja na uwanja basi jambo la msingi ni kufanya maboresho katika eneo hili muhimu.

  Previous articleDUH! RONALDO AAMBIWA NI MZEE SANA
  Next articleNAMNA SIMBA WALIVYOICHAPA 3-0 RED ARROWS KWA MKAPA