KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison imeelezzwa kuwa ameshinda kesi iliyopelekwa na Klabu ya Yanga katika Mahakama ya usuluhishi wa Michezo (CAS).
Yanga walipeleka kesi hiyo CAS baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Kamati ya Haki na Maadili na Hadhi ya Wachezaji ambayo ilitoa hukumu kuwa mkataba wa Yanga na Morrison ulikuwa na mapungufu hivyo ikaruhusu mchezaji aamue timu ambayo atakwenda.
Kwa upande wao Yanga wamekuwa wakisisitiza kuwa Morrison ni mchezaji wao halali. Morrison alisajiliwa Yanga katika dirisha dogo 2019/2020, ambapo aliitumikia kwa miezi kadhaa kabla ya kutimkia Simba.