UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa umepokea taarifa kuhusu shauri la kesi ya mchezaji wao wa zamani Bernard Morrison na kubainisha kwamba maamuzi ya CAS wameyapokea ila hayapo upande wao.
Pia Yanga wamewaomba mashabiki wa timu hiyo kusonga mbele na kuangalia mambo ya muhimu.