Home Sports MKWANJA WA SPORTPESA JACPOT BONUS WATOLEWA NI MREFU KWELI

MKWANJA WA SPORTPESA JACPOT BONUS WATOLEWA NI MREFU KWELI

MKAZI wa Bukoba wilaya ya Muleba Juhudy Stewaty (21)
ameibuka mshindi wa Jackpot Bonus baada ya kubashiri kwa
usahihi mechi 12 kati ya 13 na kujishindia kiasi cha shilingi
11,049,185.

Akizungumzia ushindi wake Juhudy amesema “Ninafuraha
kubwa sana kuibuka mshindi kwani kupitia pesa hii itanisaidia
kwenye mambo mbalimbali.

“Nilianza kucheza na SportPesa tangu mwaka 2018 hivyo ni
miaka mitatu sasa na niliifahamu hii kampuni kupitia rafiki
yangu wa karibu. Nilikuwa nikiona akiweka 500/- na kushinda
hadi elfu 40 nikashawishika sana na kuamua kuanza
kucheza.

“Ukiachilia ushindi huu mkubwa tangu nianze kucheza
nimewahi kushinda pesa kupitia ubashiri wa mechi moja
moja lakini pesa kubwa niliyowahi kushinda ni shilingi 7700
tu.

“Sikuwahi kukata tamaa hata siku moja kwenye kubashiri
nikiamini ipo siku nitashinda Jackpot ndipo nilipoanza
kuweka mikeka miwili au mitatu kwa Jackpot moja na
kushinda hii bonus hatimae imekuwa hivi.

“Mipango niliyonayo na pesa hizi ni mikubwa ikiwemo
kununua viwanja nyumbani ili niweze kuwekeza, kufungua
biashara ya nguo ambayo itaniendeshea maisha yangu ya kila siku na kuniingizia kipato na la mwisho kabisa ni kufunga
ndoa.”

Akizungumza upande wa SportPesa Mkurugenzi wa Utawala
na Udhibiti, Tarimba Abbas amesema hii ni vizuri sana kuona
tunaweza kubadili maisha ya vijana wadogo na kuinua kipato
chao.

Kupitia SportPesa tumeendelea kuwazawadia wateja wetu
zawadi mbalimbali na ndio maana hata kwa wanaobashiri
jackpot na wakapatia kwa usahihi kuanzia mechi 10 basi
watapata bonus za viwango mbalimbali kulingana na ubashiri
wao.

“Napenda kutoa rai kwa vijana kushiriki katika michezo
mbalimbali maana kubet sio uhuni bali inahitaji uelewa wa
michezo na ufuatiliaji pia ili uweze kupatia ubashiri wako”

Previous articleSIMULIZI YA ALIYEPONA UGONJWA ULIOKUWA UKIMSUMBUA
Next articleREKODI MWANZO MWISHO LIGI KUU BARA