Home Sports SIMBA YAICHAPA MABAO 3-1 RUVU SHOOTING

SIMBA YAICHAPA MABAO 3-1 RUVU SHOOTING

KIKOSI cha Simba leo Novemba 19 kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwenye mchezo wa leo ambao ulikuwa umegawanywa kwa vipindi viwili ofauti Simba ilikuwa bora kipindi cha kwanza na iliweza kufunga mabao yote matatu kupitia kwa Meddie Kagere dakika ya 17 na 36 pamoja na Kibu Dennis ambaye alipachika bao dk 44.

Kipindi cha pili kilikuwa ni mali ya Ruvu Shooting ambao waliweza kucheza kwa utulivu mkubwa na walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Elias Maguli aliyepachika bao dk 70.

Nyoni hakuwa na bahati leo kwa kuwa mikono mia ya Mohamed Makaka iliweza kuzuia penalti aliyopiga dakika ya 71 baada ya Kibu kuchezewa faulo ndani ya 18.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Simba imeweza kusepa na pointi tatu na ushindi wa mabao matatu ukiwa ni mshindi mkubwa kwa Simba msimu huu kwa kuwa kwenye mechi za awali ilikuwa inashinda bao mojamoja.

Inafikisha pointi 14 inabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kinara ni Yanga mwenye pointi 15.

Pia rekodi ya clean sheet ya Manula imetibulwa na Maguli ambaye amemtungua Manula Uwanja wa CCM Kirumba.

Previous articleKIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA RUVU
Next articlePABLO AZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA,CHAMPIONI JUMAMOSI