Home Sports NAHODHA WA YANGA ACHEKELEA KURUDI BONGO

NAHODHA WA YANGA ACHEKELEA KURUDI BONGO

NAHODHA wa zamani wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, amefunguka kuwa anafurahi kurudi Tanzania na kucheza soka kama ilivyokuwa awali.

 

Papy alisema Tanzania ni nchi ambayo aliishi kwa upendo, furaha na amani na amekuwa na marafiki wengi ambao alikutana nao akiwa anacheza Yanga.

Tshishimbi amerejea tena Tanzania na kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu yaKitayose FC ya Tabora inayoshiriki Championship akiungana na nyota aliyepita Simba, Deo Kanda.

 

Papy alisema: “Nimefurahi kurudi tena Tanzania, sehemu ambayo niliishi vizuri na kupata marafiki wengi bado niko katika ubora, naahidi kuisaidia timu kufikia malengo ya kupanda daraja.

“Nimeshamalizana na hiyo timu, kazi yangu ni soka, siwezi kuchagua timu wala daraja la timu nitakayosajiliwa, naangalia maslahi kwanza.”

Previous articleMWENDO WA USHINDI TU YANGA
Next articlePABLO AGOMEA BUTUABUTUA NDANI YA SIMBA