Home Sports MWENDO WA USHINDI TU YANGA

MWENDO WA USHINDI TU YANGA

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Koha Mkuu, Nasreddine Nabi kimeweza kuweka rekodi matata ya kucheza mechi 8 ambazo ni dakika 720 bila kupoteza huku kikifunga jumla ya mabao 13 na kufungwa mabao mawili.

Nyota wake wawili wote kibindoni wametupia mabao matatumatatu kwenye mechi walizocheza ambao ni Feisal Salum na Jesus Moloko huku baba lao akiwa ni Fiston Mayele mwenye mabao manne na pasi moja ya bao kama Fei.

Kwa msimu wa 2021/22 mwendo wake ulianza Septemba 25 iliposhinda bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ulikuwa ni wa Ngao ya Jamii na bao lilifungwa na Mayele kwa pasi ya Farid Mussa.

Walipokutana na Kagera Sugar ilishinda kwa bao 1-0, Uwanja wa Kaitaba ilikuwa Septemba 29 na mtupiaji wa bao la kwanza ndani ya kikosi hicho kwenye ligi alikuwa ni Feisal.

Kete ya tatu ilikuwa Yanga 1-0 Geita Gold, Uwanja wa Mkapa ilikuwa Oktoba 2 kwenye mchezo huu Moloko alitupia bao la kwanza kwa pasi ya Yacouba Songne.

Kituo cha nne ilikuwa KMC 0-2 Yanga, Uwanja wa Majimaji, Songea ilikuwa Oktoba 19 katika mchezo huu  Mayele alitupia bao la kwanza kwenye ligi kwa pasi ya Feisal ambaye naye alifunga bao lake la pili kwenye ligi kwa pasi ya Mayele.

Kituo cha tano ilikuwa Yanga 2-0 Azam FC, Uwanja wa Mkapa ilikuwa Oktoba 30 kwenye mchezo huu Mayele alifunga bao la pili kwenye ligi kwa pasi ya Kibwana Shomari na Moloko alifunga bao la pili kwa pasi ya Yacouba.

Mchezo wa sita ilikuwa Yanga 3-1 Ruvu Shooting, Novemba 2 kwenye mchezo huu Feisal alifunga bao lake la tatu, Djuma Shaban alifunga bao lake la kwanza kwa penalti na Tonombe Mukoko alifunga bao lake la kwanza kwa pasi ya Farid Mussa ambaye anakuwa na jumla ya pasi mbili za mabao.

Novemba 9,ulikuwa mchezo wa saba na ulikuwa wa kirafiki mbele ya Mlandege 0-1 Yanga ambapo Heritier Makambo aliweza kupachika bao katika mchezo huu na kuwajaza mashabiki wa Zanzibar ikiwa ni bao lake la kwanza akiwa visiwani.

Mwendelezo uliendelea kwa mara nyingine tena Novemba 12, mbele ya KMKM 1-2 Yanga, Uwanja wa Amaan na ni Mayele alipachika bao moja na kumfanya afunge jumla ya mabao manne  na Moloko alipachika bao moja na kumfanya atupie jumla ya mabao matatu huu ulikuwa ni mchezo wa 8 uliokamilisha dakika 730 bila kupoteza kwa Yanga.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO
Next articleNAHODHA WA YANGA ACHEKELEA KURUDI BONGO