>

URENO WANYOOSHWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA

KATIKA mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia wakiwa kundi A, Ureno walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Serbia wakiwa na Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa anapewa nafasi ya kufanya maajabu.

Mabao ya Dusan Tadic dakika ya 33 na Aleksandar Mitrovic dakika ya 60 kwa Serbia yalitosha kutibua mipango ya Ureno iliyoanza mapema kabisa kupitia kwa Renato Sanches dakika ya pili.

Wakiwa ndani ya Estadio da Luz Ureno walipiga jumla ya mashuti 9 na ni matatu yalilenga lango huku Serbia ikipiga mashuti 11 na matatu yalilenga lango pia Serbia walikuwa wakiwashambulia Ureno bila kuchoka kwa kuwa walipiga kona 10 huku wapinzani wao wakipiga kona tatu.

Ushindi huo unaifanya Ureno kubaki na pointi 17 ikiwa nafasi ya pili katika kundi A huku Serbia ikiwa ni namba moja na pointi zake ni 20 na namba tano ni Azerbaijan yenye pointi moja zote zikiwa zimecheza mechi 8 na matumaini ya Ureno kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar yamehamia kwenye mchezo wa playoffs unaotarajiwa kuchezwa Machi,2022.