Home Sports POLISI TANZANIA WAPO KAMILI KWA USHINDANI

POLISI TANZANIA WAPO KAMILI KWA USHINDANI

KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini ameweka wazi kwamba malengo ya timu hiyo ni kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara ili kuweza kuwa ndani ya tano bora kwa msimu wa

Kocha huyo mwenye tuzo ya kocha bora wa mwezi Septemba baada ya kuanza ligi kwa mwendo wa kasi bado timu hiyo ambayo kipa wao namba moja ni Metacha Mnata ni moja ya timu ambayo ipo kwenye mwendo bora ndani ya ligi

Ikiwa imecheza jumla ya mechi tano ndani ya dakika 450 imefunga mabao 7 na kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu baada ya kukusanya jumla ya pointi 10.

Kocha Malale amesema:”Ushindani ndani ya ligi ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata matokeo hilo tunalijua hivyo ni lazima tuweze kupambana ili kupata matokeo na inawezekana kutokana na wachezaji kutimiza majukumu yao kwa wakati.

“Wachezaji wanahitaji pongezi na nina amini kwamba wataendelea kuwa kwenye mwendo mzuri ndani ya ligi hivyo ni jambo la kusubiri na kuona namna itakavyokuwa,”.

Mchezo ujao kwa Polisi Tanzania ni dhidi ya Coastal Union ya Tanga na itakuwa Novemba 19, Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Previous articleMECHI ZA SIMBA V YANGA, KADI NYEKUNDU NJENJE
Next articleKOCHA SIMBA AWAAMBIA WASAJILI KIUNGO