Home Sports KOCHA SIMBA AWAAMBIA WASAJILI KIUNGO

KOCHA SIMBA AWAAMBIA WASAJILI KIUNGO

ALIYEKUWA Kocha wa Viungo wa Simba, Mtunisia, Adel Zrane, amefunguka kuwa anaamini kama Simba inahitaji kutetea ubingwa wake msimu huu, basi ni lazima wahakikishe wanavunja benki kwenye dirisha dogo la usajili na kuongeza angalau kiungo mchezeshaji mmoja mwenye uwezo mkubwa.

 

Zrane, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes na aliyekuwa kocha wa makipa, Milton Nienov Oktoba 26, mwaka huu waliachana na Simba kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

 

Katika dirisha la usajili la mwezi Agosti mwaka huu Simba ilikamilisha usajili wa nyota wapya 10 huku ikikubali kuwaachia Clatous Chama aliyejiunga na RS Berkane na Luis Miquissone aliyejiunga na Al Ahly, hali ambayo kwa kiasi kikubwa imetajwa kama sababu ya Simba kuanza kwa kusuasua msimu huu.

 

Zrane alisema: “Katika kipindi cha dirisha la usajili la mwezi Agosti mwaka huu, Simba ilifanya usajili mzuri sana lakini changamoto kubwa ilikuwa ni ishu ya kuzoea mazingira na ndiyo maana kumekuwa na hali ya kusuasua.

 

“Hivyo kwa upande wangu naamini wakati Simba wakiendelea kuwavumilia nyota wapya, wanapaswa kusajili angalau kiungo mmoja mchezeshaji atakayekuwa na uwezo mkubwa kwa ajili ya kuongeza nguvu zaidi.”

Kikosi hicho kwa sasa chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco atakosa huduma ya Clatous Chama na Luis Miquissone ambao kwa sasa wamesepa kupata changamoto mpya.

Luis yupo zake ndani ya Al Ahly na Chama yupo zake ndani ya RS Berkane.

Chanzo:Championi

Previous articlePOLISI TANZANIA WAPO KAMILI KWA USHINDANI
Next articleDEAN SMITH APATA DILI JIPYA