VIGOGO wa Ligi Kuu Bara, Simba ambao ni mabingwa watetezi pamoja na Yanga ambao ni mabingwa wa kihistoria wakiwa na mataji 27 ya ligi wakiwa kwenye mechi zao kwa msimu wa 2021/22 kadi imekuwa ni jambo la kawaida.
Hii inatokana na ugumu wa mechi hizo pamoja na wachezaji kutumia nguvu kubwa katika kusaka ushindi jambo ambalo linafanya wakati mwingine zigo kuwaangukia waamuzi kwamba wanazibeba timu hizi mbili.
Wakati mwingine kadi zinaonyeshwa ili kupunguza ile presha ila mwisho wa siku hawa vigogo wanaingia kwenye rekodi ya timu ambazo zimesababisha kadi za kutosha kwenye mechi zao.
Hapa Championi Jumatatu linakuletea mwendo wa mechi tano ambazo ni dakika 450 hali ilivyokuwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu:-
Simba
Septemba 28
Mchezo wa ufunguzi kwa Simba ulipigwa mpira wa nguvu kubwa mwanzo mwisho huku Simba wakionekana kupata tabu mwanzo mwisho mbele ya Biashara United.
Baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Biashara United 0-0 Simba ilikuwa Uwanja wa Karume, Mara.Mwamuzi wa kati Emmanuel Mwandembwa alitoa jumla ya kadi tatu za njano.
Oktoba Mosi
Ushindi wa kwanza Simba iliupata Dodoma mbele ya Dodoma Jiji 0-1 Simba, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma, mwamuzi Joseph Akamba alitoa jumla ya kadi 2 za njano zilizoleta kadi nyekundu kwa mchezaji wa Dodoma Jiji alikuwa ni Agustino Nsata.
Oktoba 27
Simba 1-0 Polisi Tanzania, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo huu mwamuzi wa kati alikuwa ni Abel William alimuonyesha kadi nyekundu Juma Ramadhan kwa kuwa alionyeshwa kadi mbili za njano.
Oktoba 31
Simba 0-0 Coastal Union, hapa mwamuzi wa kati Raphael Ikambi alitoa jumla ya kadi mbili nyekundu moja kwa mchezaji wa Simba, Henock Inonga alionyeshwa kadi ya moja kwa moja kwa kumpiga kichwa mchezaji wa Coastal Union na moja kwa nyota wa Coastal Union Benedickto Jacob huyu alionyeshwa kadi mbili za njano.
Novemba 3
Simba 1-0 Namungo FC, Uwanja wa Mkapa, mwamuzi wa kati alikuwa ni Nassoro Mwichui alitoa kadi nyekundu kwa mchezaji wa Namungo FC, Abdulaziz Makame kwa kosa la kumchezea faulo nyota wa Simba Shomari Kapombe.
Yanga
Yanga 1-0 Geita Gold, mwamuzi wa kati Ahmed Arajiga alionyesha kadi nne za njano kwenye mchezo huu na Yanga ilisepa na pointi tatu.
KMC 2-0 KMC
Oktoba 19, mwamuzi wa kati Omary Mdoe alimuonyesha kadi moja ya njano mchezaji wa Yanga ambaye alikuwa ni Yannick Bangala kwa kosa la kumchezea faulo mchezaji wa KMC.
Yanga 2-0 Azam FC
Oktoba 30 ilikuwa dabi ya presha kubwa na mwamuzi Herry Sasii alimuonyesha kadi ya njano Khalid Aucho.
Novemba 2
Yanga 3-1 Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa, mwamuzi wa kati Emmanuel Mwandembwa alimuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Santos Mazengo kwa kosa la kumchezea faulo mshambuliaji Fiston Mayele.
Maneno ya makocha
Kocha Mkuu wa Coastal Union,Melis Medo alisema kuwa wachezaji wake wanacheza kwa nidhamu hivyo suala la kadi hilo waamuzi wanaweza kulizingumzia kwa undani sababu ipo kwenye nini.
Malale Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania aliweka wazi kuwa yote ambayo yalitokea uwanjani anamuachia Mungu.
Hemed Morocco, Kocha Mkuu wa Namungo FC alibainisha kuwa anaamini mchezo wao ulimalizwa na maamuzi ya mwamuzi.
ReplyForward |