Home Sports KOCHA DR CONGO ATABIRI MATOKEO MECHI YA LEO

KOCHA DR CONGO ATABIRI MATOKEO MECHI YA LEO

MWINYI Zahera, aliyekuwa kocha msaidizi ndani ya timu ya taifa ya DR Congo amesema kuwa matokeo ya mchezo wa leo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia kati ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya DR Congo ni 50/50 kutokana na hesabu za timu zote mbili.

 

Mchezo wa kwanza walipokutana nchini DR Congo timu zote mbili zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 hivyo mchezo wa leo timu zote mbili zitakuwa na kazi ya kuonyeshana ubabe.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na mashabiki wataruhusiwa lakini wameambiwa kwamba ni muhimu kufuata taratibu za kujikinga na Corona.
  Zahera kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi masuala ya Vijana katika Klabu ya Yanga amesema kuwa hakuna mwenye uhakika wa ushindi wa mchezo leo asilimia 100 zaidi ya kila timu kuwa na asilimia 50.
“Ujue mchezo wa kwanza walipokutana ugenini timu ya DR Congo iliwachukulia kawaida Stars na wachezaji ambao walikuwa wanajulikana ni wachache ikiwa ni pamoja na Mbwana Samatta walikuwa wanajua kwamba wachezaji wengi wa Stars ni wa ndani kwa kuwa walishacheza nao watakuja kwa mtindo tofauti.
“DR Congo wanajua kwamba ili waweze kusonga mbele lazima washinde wakifungwa wanatoka katika mashindano na Stars nao wanahitaji kushinda ili kusonga mbele hapo unaona namna gani mchezo utakuwa mgumu kwa timu zote mbili.
“Naweza kusema kwamba hata kama Stars itakuwa ipo Uwanja wa Mkapa basi haimaanishi kwamba watashinda kwa wepesi ni moja ya mchezo mzuri kwa kuwa unazikutanisha timu ambazo zinasaka ushindi.
“Pia hata hao DR Congo nao wameongeza uzito kwenye kikosi na kuwaita wachezaji wenye uzoefu hivyo kila atakayeweza kutumia makosa ya mpinzani atapata ushindi,” alisema Zahera.
Previous articleNAFASI YA STARS KUFUZU KOMBE LA DUNIA NI 50/50
Next articleMAKIPA BONGO NA MIGUSO YAO YA MAANA