NAFASI ya Tanzania kuhusu kufuzu Kombe la Dunia kweda Hatua ya Play off naiona ni 50/ 50 yaani lolote linaweza kutokea kwenye mpira maana hawako katika nafasi nzuri sana wala mbaya kwenye msimamo wa kundi J.
Ikumbukwe kwamba kwa sasa Tanzania ni kinara wa kundi hilo akijikusanyia pointi 7 kwenye mechi 4 ambazo amekwishacheza mpaka sasa hivi , Taifa Stars ni mabao matano safu ya ushambuliaji imetupia na kufungwa mabao manne.
Sina shaka na kiwango cha Taifa Stars kwa mechi za hivi karibun ukizingatia ubora kwa timu pinzani za Taifa Stars kwenye kundi J nikiwazungumzia Benin wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 7 sawa na Tanzania huku DR Congo ikishika nafasi ya 3 ikiwa na pointi tano na Madagascar wakishika mkia wakiwa na pointi 2.
Hapa ukifanya hesabu kwa haraka haraka ukimtoa Madagascar kwenye orodha ya kusonga mbele timu 3 zote zina nafasi. Kama Stars watashinda michezo yote mwili iliyobaki watafikisha jumla ya pointi 13, Benin pia akishinda michezo yote iliyobaki atafikisha jumla ya point 13 na DR Congo akiziombea mabaya Stars na Benin akishinda michezo yote 2 iliyobaki atafikisha pointi 11 .
Kiufundi Stars wamekuwa na chati ya kupanda na kushuka pengine hii ni kwa timu nyingi za Africa ambazo zimeporomoka sana kwenye ubora wao Afrika ukitoa mataifa kama Senegal, Morroco na Misri ambao wamekuwa na muendelezo mzuri wa ubora wao huku wakiwa wameshafuzu hatua inayofuata ila Misri anahitaji pointi kadhaa kufuzu hatua inayofuata.
Dua na sala kwa Watanzania ziwe kwa Stars leo ambayo ina kibarua cha kucheza na DR Congo Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.
Imeandikwa na Ibra da 01
Mwl wa Chandimu