Home Sports YACOUBA APELEKWA TUNISIA

YACOUBA APELEKWA TUNISIA

YACOUBA Songne, mshambuliaji wa kikosi cha Yanga raia wa Burkina Faso, amepelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.

Songne anaesumbuliwa na jeraha la goti huenda akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu kutokana na ukubwa wa jeraha hilo.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikishinda kwa mabao 3-1 hakuweza kuyeyusha dakika zote 90 kwa kuwa aliumia kipindi cha kwanza.

Nafasi yake ilichukuliwa na kiungo mshambuliaji Said Ntibanzokiza ambaye aliweza kuonekana akicheza mchezo wa ligi msimu wa 2021/22 kwa mara ya kwanza.

Nyota huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi hivyo kuwa kwake nje kutampa nafasi nyingine kocha huyo kumtafuta ambaye atachukua mikoba yake ila kwa namna kikosi cha Yanga kwa sasa kilivyo huenda haitampasua sana kichwa.

Mpaka sasa kwenye ligi, rasta huyo ametoa pasi mbili za mabao na yote yalifungwa na Jesus Moloko.

Previous articleSTARS KUKWEA PIPA BAADA YA MECHI
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI