>

MANCHESTER UNITED WAMECHANA MKEKA

KLABU ya Manchester United imekubali kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Old Trafford.

Bao la kujifunga la nyota wao Eric Bailly dakika ya 7 liliwapotezea umakini United ambao waliruhusu kufungwa bao la pili ilikuwa dakika ya 45 kupitia kwa nyota Bernardo Silva na ilikuwa ni dakika ya 45.

Mpaka muda wa mapumziko United ilikuwa nyuma kwa mabao hayo mawili na hata waliporudi ngoma ilikuwa nzito kwao kuweza kupata mabao kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Licha ya kupoteza pia United haikuwa imara kwenye suala ushambuliaji ambapo hawakufanya hatari nyngi kwenye lango la mpinzani wake City aliyekuwa akicheza mpira wa pasi nyingi ugenini.