RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO

NOVEMBA 2,2021 Ligi Kuu Tanzania Bara inazidi kushika kasi ambapo ushindani umekuwa mkubwa tofauti na msimu uliopita.

Leo viwanja viwili vitakuwa na burudani tosha kwa mashabiki wao huku wachezaji wakionyesha kile ambacho wamefundishwa na makocha wao katika muda wa maandalizi.

Ni mchezo kati ya Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 12 kwenye msimamo wa ligi na itakutana na Ruvu Shooting 8 na pointi 6.

Mchezo huu utachezwa Uwanja wa Mkapa itakuwa ni kuanzia saa 12:15 na tayari tiketi zinauzwa kwa wakati huu hivyo ni suala la mashabiki kuweza kutimiza wajibu wao na kwa wale walio mbali waweza kuitazama Azam TV.

Mchezo mwingine ni kati ya Azam FC iliyo nafasi ya 11 na pointi 4 itakuwa dhidi ya Geita Gold iliyo nafasi ya 13 na pointi 2 itakuwa ni saa 2:30 usiku.