Home Sports YANGA YAITUNGUA AZAM KWA MKAPA

YANGA YAITUNGUA AZAM KWA MKAPA

DAKIKA 90, zimemalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa huku Yanga wakiibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa NBC Ligi Kuu Bara.

 

Bao la kwanza la Yanga limefungwa na mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 36 kwa assist ya Shomari Kibwana, ya mchezo baada ya makosa ya mabeki wa Azam wakiongozwa na Yvan Mballa na Daniel Amoah.

 

Yanga ambao ni wenyeji wameonekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo tofauti na Azam ambao wanacheza kwa tahadhari huku wakishambulia kwa kushitukiza.

 

Sehemu kubwa ambayo Kocha wa Azam George Lwandamina amefanikiwa katika kipindi cha kwanza ni uteuzi wa kikosi hasa uwepo wa kiungo Kenneth Muguna ambaye ameonekana kupambana vyema na Yannick Bangala kwenye eneo la katikati ya Uwanja.

 

Ushindi huu wa unakuwa muendelezo mzuri kwa Yanga msimu huu ambayo sasa imeonekana kuimarika kuanzia mabeki, viungo mpaka safu ya ushambuliaji. Yanga sasa wanaongoza Ligi Kuu wakiwa na pointi 12.

Previous articleTUMAINI MABIGWA MERIDIAN BET STREET SOCCER BONANZA
Next articleMASTAA YANGA WAOGA MAMILIONI, SIMBA WANA JAMBO LAO