Home Sports NYOTA SIMBA AIPA UBINGWA YANGA

NYOTA SIMBA AIPA UBINGWA YANGA

NYOTA wa zamani wa Klabu ya Simba, raia wa Ghana Nicholas Gyan amesema kuwa Yanga ya msimu huu ni bora kuliko Yanga zote za misimu minne iliyopita na ina nafasi ya kutwaa ubingwa.

Gyan alisema Simba hawatakiwi kubweteka badala yake wawe makini kwa kuwa mwenendo wa Yanga ya msimu huu unaonekana bora sana na kila mchezo wanaocheza wanaonekana kubadilika na kuwa bora zaidi.

Gyan ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha DTB FC kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, aliwahi kutwaa mataji mawili akiwa na Simba, msimu wa 2017-18 na 2018-19 kisha akatemwa baada ya kukosa nafasi ya kudumu.

Akizungumza na Championi Jumatatu Gyan alisema: “Huwa natazama mechi za Simba na Yanga kama ambavyo imekuwa desturi ya Watanzania wengi. Yanga wanaonekana kuwa wanahitaji kitu msimu huu.

“Na kwa namna ambavyo walivyo bora naona wanakwenda kufanya mambo makubwa sana, siyo Yanga ile ya misimu minne nyuma, hii iko bora zaidi na Simba wanatakiwa kuwa makini zaidi kwa kuwa mwisho wanaweza kutoka kapa,” .

Yanga imecheza mechi tatu na kibindoni imekusanya pointi tisa huku ikiwa imefunga mabao manne kwenye mechi hizo na kinara wa utupiaji ni mzawa Feisal Salum mwenye mabao mawili na pasi moja ya bao kibindoni.

Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Simba ambao kwa sasa wananolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery baada ya panga kupita kwenye benchi la ufundi kwa kumchimbisha Didier Gomes aliyekuwa kocha mkuuu wa timu hiyo.

Previous articleKOCHA MPYA SIMBA APEWA SAA 48,GOMES AITAJA YANGA
Next articleMOUNT ACHEKELEA KUWATUNGUA NORWICH